Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal Union yawatema watatu

Coastal Union Yawatema Watatu.jpeg Coastal Union yawatema watatu

Tue, 26 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Coastal Union tayari imeanza kuwatema kikosini baadhi ya nyota wake kadhaa ambao wameshindwa kuonesha kiwango kilichotarajiwa tangu wajiunge na klabu hiyo kutoka Pwani ya Kaskazini Mashariki mwa Tanzania.

Hadi sasa tayari wachezaji watatu [Mapinduzi Balama, Juma Mahadh na Fran Golubic] wameshaachwa na Coastal Union katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.

Wengine ambao Coastal Union inatarajia kuwaacha ni Abilah Yacoub Salah raia wa Nigeria na Daud Salum Mbweni ambaye alikuwa Coastal Union kwa mkopo akitokea Singida Fountain Gate FC.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Coastal Union Abbas El-Sabri bado kuna wachezaji wengine ambao wanafikiria kuachana nao ukiachana na hao wachezaji watano.

Wachezaji wote waliotemwa ni mapendekezo kutoka kwenye ripoti ya Kocha Mkuu wa Coastal Union, David Ouma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live