Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal Union yaususa ubingwa Ligi Kuu

Coastal Hadharani Leo Coastal Union yaususa ubingwa Ligi Kuu

Fri, 26 Jan 2024 Chanzo: Dar24

Licha ya kuwa katika nafasi ya sita kwenye msimamo, uongozi wa Coastal Union ya Tanga umeanika malengo yake matatu makubwa huku ikijiweka pembeni kwenye mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Tayari kikosi cha Coastal Union kimeanza rasmi mazoezi yake kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani, ulioko Tanga ili kujiweka imara na mechi za ligi kuu inayotarajiwa kuendelea tena hivi karibuni.

Mabosi wa timu hiyo kongwe wamelitaka benchi la ufundi kuhakikisha wanafikia malengo ya klabu hiyo.

Ofisa Habari wa Coastal Union, Abbas El-Sabri, amesema pamoja timu hiyo kutopata matokeo mazuri katika mechi za awali katika mzunguko wa kwanza, lakini ushindi waliopata kwenye michezo ya hivi karibuni imewafanya kutotoka katika kiu ya kufanya vizuri ya kila mchezaji waliyemwongeza kwenye kikosi chao.

“Lengo letu la kwanza ni kumaliza katika moja kati ya nafasi nne za juu, pili ni kukata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao na tatu ni kutwaa Kombe la Shirikisho ‘ASFC’, tunaweza kufanikiwa yote, mawili au moja kati ya hilo, lakini haya ndiyo malengo yetu,” amesema El-Sabri.

Ameongeza ana uhakika wana uwezo wa kufikia malengo hayo kutokana na usajili bora waliofanya kipindi cha dirisha dogo na wachezaji wapya waliosajiliwa na Coastal Union kipindi cha dirisha dogo la usajili ni pamoja na Mganda David Ouna, Salim Aiyee kutoka Mbuni FC na Mkongomani Kasindi Paulin.

Mabingwa hao wa mwaka 1988 wana pointi 19 baada ya kucheza michezo 14, wakishinda mechi tano, sare nne na kupoteza michezo mitano huku kibindoni wakiwa na mabao 11 ya kufunga.

Chanzo: Dar24