Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal Union yambana Matampi

Ley Matampi Pp Ley Matampi.

Sat, 8 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa klabu ya Coastal Union ya Tanga bado umeendelea kusisitiza golikipa Ley Matampi bado ni mali yao na kumtaka mkongo huyo kuonyesha mkataba wake wa mwaka mmoja anaosisitiza kuusaini kabla ya kuanza kuichezea timu hiyo msimu uliopita.

Mara baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu Tanzania bara hivi karibuni, kumeibuka mvutano wa kimkataba kati ya uongozi wa klabu hiyo golikipa Ley Matampi wakivutana juu ya uhalali wa mkataba wa nyota huyo.

Golikipa huyo raia wa Kongo ameweka wazi kuwa amemaliza mkataba wa kuichezea timu hiyo kwa kuwa mkataba wake na timu hiyo ulikuwa wa mwaka mmoja.

Hata hivyo, uongozi wa Coastal Union ukiongozwa umemtaka golikipa huyo aonyeshe mkataba huo wa mwaka mmoja anaodai kusaini.

Akizungumza nasi jana, Katibu Mkuu wa klabu hiyo Omar Ayoub,alisema hawana nia ya kumzuia Matampi kuondopka kama amepata timu, lakini wanataka tararibu na sheria zifuatwe.

"Sisi kama Coastal Union tunasema Matampi bado ana mkataba na sisi, sasa yeye kama anasema alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja tu, auonyeshe, sisi nyaraka zote tunazo," alisema.

Alisema hata kama kuna timu inamuhitaji hawatasita kumruhusu kama watafuatwa na kukubaliana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live