Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal Union yalaani mijadala ya Fair Competition

Coastalunionfc 117705136 319789382407795 6472219774004032326 N 1 (600 X 600) Costal Union, Miongoni mwa klabu zinazodhaminiwa na GSM

Tue, 9 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Klabu ya Coastal Union umetoa taarifa ya kusikitishwa na Mjadala unaoendelea hivi sasa kwenye mitandao ya kijamii, uliopachikwa jina la Fair Competition ambao unaihusu kampuni ya GSM.

Kampuni ya GSM inatajwa kwenye mjadala huo, kufuatia udhamini/ufadhili iliouweka kwenye klabu za Coastal Union, Young Africans na Namungo FC.

Taarifa iliyotolewana Uongozi wa Coastal Union na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii leo Jumanne (Novemba 09) imeeleza kuwa, Mjadala huo hauna afya na hauleti tija kwenye soka la Tanzania kwani utafanya kudumaza soka la Tanzania kutokana na Wadhamini kujiondoa.

Kutokana na hali hiyo Uongozi wa Coastal Union umewataka wachambuzi pamoja na watu waliopo kwenye vyombo vya habari kutumia nafasi walizonazo kuwashawishi wawekezaji kwenye soka la Tanzania na sio kuwavunja moyo.



Chanzo: www.tanzaniaweb.live