Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal Union yaiadhibu Ruvu Shooting

Ac6b3d4aa0cf37542c476e22af169491.jpeg Coastal Union yaiadhibu Ruvu Shooting

Sun, 18 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TIMU ya Coastal Union imeutumia vema uwanja wa nyumbani wa Mkwakwani baada kuifunga Ruvu Shooting kwa mabao 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara jana.

Kwa matokeo hayo Coastal Union imepanda hadi nafasi ya tisa kutoka nafasi ya 11 baada ya kufikisha pointi 33 ikicheza michezo 26 na Ruvu Shooting inabaki katika nafasi ya nane ikiwa na pointi 34 baada ya kucheza michezo 25.

Katika mchezo huo ambao ulianza kwa kasi Ruvu Shooting ndio walioanza kupata bao dakika ya 20 likifungwa na Fully Maganga lakini Rashidi Mohamed aliisawazishia Coastal Union dakika ya 42 na kwenda mapumziko kwa sare ya 1-1.

Kipindi cha pili Coastal Union walionesha dhahiri kuwa wana jambo lao na dakika ya 63, Ayoub Abdallah aliifungia timu yake bao la pili ambalo lilidumu hadi dakika 90 zinamalizika.

Mchezo uliopita Coastal Union iliifunga Biashara 1-0 katika Uwanja wa Karume, Mara ikiwa ni timu ya tatu kuifunga nyumbani baada ya Simba na Yanga.

Katika mchezo mwingine uliochezwa Uwanja wa Jamhuri Morogoro, Mtibwa Sugar wakiwa nyumbani walitoka sare ya 1-1 na Kagera Sugar.

Katika mchezo huo Mtibwa walianza kupata bao dakika ya 25 lililofungwa na Japhary Kibaya lakini Yusuf Mhilu aliisawazishia Kagera Sugar dakika ya 44 na kwenda mapumziko wakiwa nguvu sawa.

Kipindi cha pili kila timu ilishambulia lango la mpinzani ili kupata bao lakini mabeki wa timu zote walikuwa makini kuhakikisha ngome yao haipenyeki kirahisi na kufanya mchezo kumalizika kwa 1-1.

Kwa matokeo hayo Kagera Sugar imefikisha pointi 27 katika nafasi 13 baada ya kucheza michezo 26 na Mtibwa Sugar inasalia katika nafasi ya 15 ikiwa na pointi 25 baada ya kucheza michezo 25.

Timu hizi zote zipo katika hali mbaya kwani mmoja wapo anaweza kushuka daraja na mwingine kuangukia kucheza ‘play off’ endapo zitaendelea kuwa na matokeo mabovu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz