Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal Union yahamia kwa Duke Abuya

Duke Abuya SFG (600 X 437) Duke Abuya

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Coastal Union imetajwa kuwa iko mbioni kumsajili kiungo mshambuliaji raia wa Kenya anayeichezea Klabu ya Singida Black Stars, Duke Abuya, ikiwa ni mikakati ya maandalizi ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa kwa sasa ipo kwenye mazungumzo na mchezaji huyo ambaye kwa sasa amemaliza mkataba na klabu yake hiyo.

Hata hivyo, habari zinaeleza klabu yake hiyo ipo kwenye jitihada kubwa za kumshawishi kubaki, lakini mwenyewe anaonekana kutaka kwenda kucheza michuano ya kimataifa kwa lengo la kujiweka sokoni.

"Tuko kwenye mazungumzo naye, hatujamaliza, lakini ameonyesha kukubali na anataka kucheza mechi za kimataifa na sisi tumemwambia aje kwetu, akicheza Kombe la Shirikisho ataonekana, lakini klabu yake nayo inamshawishi abaki, mwisho wa siku tutaona, lakini tuna nafasi kubwa ya kumpata," alisema mtoa taarifa kutoka ndani ya Coastal Union.

Hivi karibuni, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Abbas El Sabri, alisema wako kwenye mikakati kabambe kuhakikisha wanasajili wachezaji bora na wazoefu wa mechi za kimataifa, ili kushiriki vema michuano hiyo na haiendi kusindikiza.

Mmoja wa wachezaji ambao alikiri kuwa nao kwenye mazungumzo ni beki wa zamani wa AS Vita ya DR Congo na Yanga, Djuma Shaaban.

"Ni kweli tupo kwenye mazungumzo na Djuma, ni mchezaji mzuri, mzoefu katika mechi za kimataifa. Unajua tangu tulipopata nafasi ya kucheza Kombe la Shirikisho, tayari kama klabu tukatambua mahitaji yetu," alisema.

Pamoja na kumtaja mchezaji mmoja tu, lakini habari zinaeleza kuwa klabu hiyo ilikuwa kwenye mazungumzo na wachezaji Saido Ntibazonkiza aliyeachwa na Simba, pamoja na winga wa zamani wa Yanga na RS Berkane ya Morocco, Tuisila Kisinda ambaye amemaliza mkataba wake na klabu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live