Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal Union watinga Nusu Fainali Kombe la CRDB

IMG 0087.jpeg Coastal Union watinga Nusu Fainali Kombe la CRDB

Wed, 1 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Coastal Unión imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya ushindi wa 1-0 katika mchezo wa Robó Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano ambayo sasa inajulikana kama CRDB Bank Federation Cup baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Geita Gold leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.

Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, winga Mghana, Dennis Modzaka mwenye umri wa miaka 23 aliyefunga dakika ya 23 na sasa Wagosi wa Kaya au Wana Mangush watakutana na mshindi kati ya Azam FC na Namungo FC zitakazomenyana Mei 3 Jijini Dar es Salaam.

Coastal Union inakuwa timu ya pili kutinga Nusu Fainali ya CRDB Bank Federation Cup baada ya Ihefu SC ambayo imeitoa Mashujaa FC kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya 0-0 leo Uwanja wa LITI mjini Singida.

Ihefu itakutana na mshindi kati ya Yanga na Tabora United zinazomenyana usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live