Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal Union wao ni pesa mezani tu

Coastal Union Business Coastal wameuza wachezaji wao kam sopu na Victor Akpan

Thu, 7 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dili la Abdul Suleiman ‘Sopu’ na Victor Akpan limewapa mamilioni Coastal Union ambao wametamba kufanya usajili wa maana msimu ujao.

Kuondoka kwa mastaa wawili ndani ya Coastal Union ambayo imemaliza nafasi ya saba kwenye msimamo msimu huu kumeiingizia Sh 200 milioni timu hiyo.

Pesa hiyo imetokana na timu hiyo kuuza mastaa wake wawili kiungo Akpan ambaye anatajwa kujiunga Simba na Sopu aliyetua Azam FC.

Wawili hao walikuwa na mikataba ya kuendelea kuitumikia timu hiyo msimu ujao hivyo uongozi umefanya biashara na timu tajwa hapo juu ili kukamilisha uhamisho wa mastaa hao.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Coastal Union kimethibitisha kuwa wamevuna kiasi hicho cha pesa baada ya kukamilisha dili za wachezaji hao. Mbali na pesa hizo za usajili timu hiyo imepata Sh55 milioni kutoka kwa wadhamini wenza wa ligi ambao ni Azam Tv na kufanya wakusanye kitisha cha Sh255 milioni. Uongozi umethibitisha kupata kiasi hicho cha fedha na wataendelea kufanya biashara ya kukuza vipaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live