Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal Union waichapa Singida FG Mkwakwani

IMG 0211.jpeg Coastal Union waichapa Singida FG Mkwakwani

Sat, 11 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Coastal Union wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Jana Usiku Mei 10 Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.

Mabao ya Coastal Union yamefungwa na mshambuliaji Crispin Ngushi Mhagama (25) dakika ya 26 na kiungo Greyson Gerard Gwalala (30) dakika ya 46.

Kwa ushindi huo, Coastal Union inafikisha pointi 37, ingawa inabaki nafasi ya nne, wakati Singida Fountain Gate inabaki na pointi zake 29 na kushuka kwa nafasi moja hadi ya 10 baada ya wote kucheza mechi 26.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: