Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal Union waibuka na ushindi Mkwakwani

Coastal Vs Mbeya Citi 1 Ushindi wa bao 1-0 iliyopata Coastal Union ya Tanga dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Mkwakwani

Sat, 18 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ushindi wa bao 1-0 iliyopata Coastal Union ya Tanga dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Mkwakwani, umeifanya ipande hadi nafasi ya 13 na kuishusha Prisons nafasi ya 14.

Licha ya Prisons kulingana pointi 22 na Coastal ipo nyuma mchezo mmoja ambapo leo itakuwa kwenye Uwanja wa Ushirika kucheza na Polisi Tanzania, isipokuwa zina tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Costal inamiliki mabao ya kufunga 19 na kufungwa 28, huku Prisons inamiliki mabao 18 na imetikiswa nyavuni mara 30.

Bao la Coastal lilifungwa dakika 10 kupitia kwa Vicent Abubakar jambo ambalo kiufundi timu hizo hazikuzidiana sana kwenye mbinu.

Katika michezo 23 ambayo Mbeya City imecheza, imeshinda mitano, sare tisa na kupoteza 10 na kukusanya pointi 24, huku kwa upande wa Coastal imeshinda mitano, sare saba na kupoteza 11 na pointi 22.

Mzunguko wa kwanza timu hizo zilitoshana nguvu kwa sare za mabao 2-2, Uwanja wa Sokoine, mabao ya Mbeya City yalifungwa na Sixtus Sabilo dakika ya 39 na 80 huku yale ya Coastal yakifungwa na Greyson Gwalala na Hamad Majimengi (Novemba 13,22).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live