Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal Union wafufukia kwa matajiri wa Singida

Sing Vs Coastal.jpeg Coastal Union ilikuwa na mfululizo wa matokeo mabaya katika michezo yake miwili iliyopita

Wed, 7 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Coastal Union imeondoka na pointi tatu baada ya kuifunga Singida Big Stars mabao 2-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, mchezo uliochezwa Uwanja wa Liti Singida.

Singida imepoteza mechi ya nne kwenye ligi msimu huu, ikiwa ni ya kwanza kupoteza kwenye uwanja wake wa nyumbani.

Mabao ya Coastal Union yalifungwa na Nimubona Emery dakika ya 28 na Vicent Abubakari dakika ya 49 huku lile la Singida Big Stars likifungwa na nahodha Deus Kaseke dakika ya 90 kwa nmkwaju wa penalti.

Kwenye mechi 15 za Singida Big Stars, imeshinda nane, sare tatu, imefungwa tatu huku ikifunga mabao 16 ikifungwa 12.

Katika mabao 14 iliyoyafunga Coastal Union, matano yamefungwa na mshambuliaji Mubarack Hamza. Coastal baada ya mchezo huo inapanda hadi nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi ikiwa imeshinda mechi nne, sare tatu na kupoteza nane.

Bao la Kaseke linakuwa la 16 kwa timu yake katika mechi 15 ambazo imecheza huku Meddie Kagere akiwa kinara wa ufungaji kwenye kikosi hicho.

Singida Big Stars imemaliza mzunguko kwa kwanza wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 27 ikishika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.

Katika mchezo huo, Mwamuzi Hussein Athumani kutoka Katavi aliwaonesha kadi za njano Vicent Abubakari, kipa Hamad Maobrouk na Gustavo Simon wa Coastal Union na kiungo Hamis Ndemla na Singida Big Stars.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live