Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal Union 'thank you' zinaendelea

Coastal Union Ligi Leo.jpeg Coastal Union 'thank you' zinaendelea

Sat, 30 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati mashabiki na wadau wa soka wakishangaa na panga linalotembezwa kwa wachezaji Coastal Union, uongozi wa timu hiyo umesema bado jambo hilo ni endelevu kuwapunguza nyota ambao hawajaridhishwa na kiwango chao kutokana na ripoti ya benchi la ufundi.

Hadi sasa Wagosi hao wa Kaya wa jijini Tanga wametimua mastaa saba katika dirisha hili dogo ikiwa haijatangaza igizo lolote jipya na kuwapa mshangao wadau na mashabiki wa timu hiyo.

Hata hivyo pamoja na panga hilo, lakini timu hiyo imekuwa bora kwa mechi za  hivi karibuni tangu wamtangaze kocha mpya,  David Ouma raia ya Kenya akiziba nafasi ya mtangulizi wake, Mwinyi Zahera aliyepelekwa timu ya vijana (U20).

Ouma aliikuta Coastal Union nafasi ya 13 kwa pointi saba, ambapo ameiongoza michezo 10 ikiwamo ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na sasa ipo nafasi ya sita kwa alama 19 baada ya kucheza mechi 14 kwenye Ligi Kuu.

Waliopewa 'Thank you' hadi sasa ni Barama Mapinduzi ambaye tayari ametambulishwa Mashujaa FC, Juma Mahadhi, Yakubu Abdulah, Fran Gulobic, Abdulswamadu, Kassim, Daud Mbweni na Konare Malienne.

Ofisa habari wa timu hiyo, Miraji Wandi amesema wanachofanya siyo cha kubahatisha bali ni mipango ya timu kutekeleza ripoti ya benchi la ufundi 'kufagia' wale ambao hawajaridhishwa na kiwango chao.

Amesema kujua wataacha wangapi bado haijaeleweka akisema pamoja na matokeo waliyopata yenye kuridhisha chini ya kocha Ouma, lakini wanatengeneza Coastal Union mpya ambayo itaendeleza makali Ligi Kuu na kombe la ASFC.

"Tulivyosajili dirisha kubwa tulikuwa na matarajio makubwa chini ya kocha Zahera, lakini baada ya Ouma kuja tumepata matokeo mazuri lakini kuna ambao viwango havijaridhisha na ndio hao tunatoa mmoja mmoja kila siku"

"Benchi la ufundi limependekeza likawasilisha ripoti kwa mwenyekiti wa kamati ya usajili Zuberi Ally hivyo huenda kadri tunavyopunguza kutakuwa na mbadala wao" amesema Wandi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live