Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal Union kumtangaza Mdhamini mpya leo

Coastal Union Wamkanda Mtu 4 0 Wamtambia Simba 'anayefuata Ajiandae' Coastal kutangaza Mdhamini mpya leo

Sat, 16 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Coastal Union imetangaza kuwa leo Jumamosi Septemba 16, 2023 itatambulisha mdhamini wake pamoja na zoezi la utiaji saini makubaliano ya udhamini kwa msimu huu wa ligi kuu ya NBC, Tanzania bara.

Kupitia taarifa yake kwa umma Coastal Union imesema zoezi hilo ambalo pia litaambatana na kuwatambulisha wadhamini wake wenza, litafanyika kuanzia saa 7:00 mchana katika hotel ya Tanga beach Jijini Tanga.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo anatarajiwa kuwa katibu mkuu wizara ya utamaduni, Sanaa na michezo Mh Said Yakub.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: