Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal Union kujipima nguvu na Singida FG leo

Coastal Union Kujipima Nguvu Na Singida FG Leo Coastal Union kujipima nguvu na Singida FG leo

Mon, 7 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wagosi wa Kaya, Coastal Union leo wanatarajia kushuka dimbani kucheza mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Singida FG katika dimba la Mkwakwani jijini Tanga.

Huu utakuwa ni mchezo mzuri kwa timu zote mbili kujipima kabla ya Ligi Kuu msimu wa 2023-24 kuanza kwani zote zinashiriki.

Kwa upande wa Singida FG, mchezo huu huwenda ukawa na faida au hasara kwao kwani wapinzani wao wa kwanza katika mechi ya Ngao ya Jamii (Simba SC) watakuwa wakiwasoma mbinu zao lakini pia huwenda faida ikawa kwao kwa uzoea uwanja ambao ndio utachezewa mechi yao ya kwanza.

Simba wao jana Agosti 6, 2023 walicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Power Dyamos ya Zambia na mara baada ya mchezo huo, wanajiandaa na mchezo huo wa Ngao ya Jamii utakaopigwa Alhamisi Agosti 10, 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live