Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal Union inajitafuta kimataifa

Zahera X Coastal Tanga Coastal Union inajitafuta kimataifa

Fri, 8 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Coastal Union umesema utahakikisha kuwa unafanya vizuri kwenye ligi kuu msimu huu ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.

Mpaka sasa kwenye ligi Coastal Union ipo nafasi ya 10 ina pointi moja baada ya kucheza michezo miwili baada ya kupoteza mchezo mmoja na kutoa sare mchezo mmoja.

Timu hiyo iliwahi kucheza fainali ya Azam Sports Federation a kugotea washindi wa pili huku ubingwa ukiwa mikononi mwa Yanga. Yanga ilishinda mchezo huo kwa penalti baada ya kufungana mabao 3-3 kwenye mchezo huo.

Timu hiyo ipo chini ya Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera ambaye aliwahi kuinoa Yanga na Polisi Tanzania kwa nyakati tofauti. Ofisa Habari wa Coastal Union, Abbas El-Sabri alisema kuwa uongozi una malengo makubwa inayofanyia kazi kwa msimu mpya.

“Tuna malengo ya kufanya vizuri kwenye ligi ili kushiriki mashindano ya kimataifa na hilo linatufanya tufikirie kumaliza ndani ya nafasi nne za juu.

“Pia tunamalengo ya kuchukua taji la Azam Sports Federation hilo linawezekana kwa kuwa tuna nia ya kushiriki mashindano ya kimataifa msimu ujao,” amesema Zahera.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live