Afisa habari wa klabu ya Coastal Union Abbas El Sabri ameweka wazi kuwa mlinzi wao Lameck Lawi bado ni mchezaji wao halali na hawatambui utambulisho waliofanywa na klabu ya Simba SC kwa mlinzi huyo.
Klabu ya Simba imetangaza kumnyakua beki wa mpira Lameck Lawi akitokea Coastal Union ya Tanga.
Swali: Kwa nini msikanushe kwenye page zenu za Coastal Union?
"Kama (Simba SC) wamemsajili Kiuhalali Lameck Lawi wapost picha akisaini, Sisi hatuwezi kupost kwenye account zetu kukanusha hiyo taarifa isiyokamilaika"
"Mtu mkeo unaweza kutangaza mke wangu mke wangu ?! Kisa tu kuna mtu mwingine alitangaza ni mke wake, Simba Wameshindwa kufuata masharti, hatumuuzi Lawi"
"Lawi ataendelea kuwa mchezaji wetu na muda si mrefu ataingia kambini," Abbas El Sabri - Afisa habari wa Coastal Union.
Sakata hilo linakuja baada ya klabu ya Simba SC kumtangaza Lawi kuwa mlinzi wao mpya.
Katika msimu uliopita, nyota huyo wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) amecheza mechi 25 akitumia dakika 2230 akiwa na uzi wa Coastal Union kwenye NBC Premier League.