Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal Union, Prisons hakuna mbabe

Prisons Pcers Coastal Union, Prisons hakuna mbabe

Tue, 7 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Pointi moja waliyovuna kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons inawabakisha Coastal Union kwenye nafasi ile ya nne.

Mei 6, 2024, Coastal Union ilikuwa na kazi ya kusaka pointi tatu dhidi ya Tanzania Prisons kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Coastal Union 0-0 Tanzania Prisons hivyo wababe hao wote wawili waligawana pointi mojamoja.

Ni pointi 34 wanafikisha Coastal Union nafasi ya nne kwenye msimamo huku Tanzania Prisons ikiwa nafasi ya sita na pointi 32 kibindoni.

Ipo wazi kwamba vinara wa ligi ni Yanga weye pointi 65 baada ya kucheza mechi 25.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live