Wagosi wa Kaya Coastal Union ya Tanga wameendelea kutopata ushindi uwanja kwenye uwanja wa nyumbani Mkwakwani katika mchezo wao wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya sare na KMC.
Coastal Union waliikaribisha KMC ambao walitoka kupoteza mchezo wao wa kwanza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania.
Katika michezo miwili Coastal Union ameambulia pointi mbili baada ya mchezo wa kwanza kutoka sare ya bao 1-1 na Azam FC huku KMC wakipata alama moja katika mechi mbili.
Kipindi cha kwanza timu zote zilionekana kushambuliana zamu kwa zamu huku na kukosa nafasi za kufunga kutokana na namna ambavyo kila timu ilihitaji matokeo katika mchezo huo.
dakika ya 18 Awesu Awesu anakosa nafasi ya kufunga baada ya shuti lake kupaa juu ya lango huku umakini wa Kaseja na Mbisa ukiwakosesha nafasi wafungaji baada ya mipira kuishia mikononi mwao.
Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kulishambulia lango la mwenzake lakini umakini wa kila safu ya ulinzi ulipelekea kushindwa kupata nafasi ya kufunga.
Dakika ya 82 Ismail Gambo anatolewa kwa kadi nyekundu ikiwa ni kadi ya njano ya pili baada ya kucheza rafu mbaya kwa mpinzani.
Kikosi cha KMCÂ Juma Kaseja, Kelvin Kijili, Ally Ramadhan, Ismail Gambo, Andrew Vicent, Hassan Kapalata, Kenny Ally, Awesu Awesu, Chalres Ilamfya, Idd Kipangwile na Emmanuel Mvuyekure
Kikosi cha Coastal Mussa Mbisa, Hance Masoud, Aman Kyata, Sossytoure Idah, Rashid Ghambo, Abdul Suleiman 'Sopu', Ngamchiya Amza, Raizin Hafidh, Vicent Aboubakar na Hamad Majimengi