Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal Biashara asubuhi, Yapanga mikakati mapema

Coastal Kambi Kocha Mkuu Coastal Union, Melis Medo

Fri, 10 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Coastal Union umeweka wazi kuwa kwa sasa upo kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22.

Ofisa Habari wa Coastal Union, Miraji Wandi ameweka wazi kuwa kila kitu kinakwenda sawa na wanaamini kwamba watafanya vizuri kwa msimu ujao.

"Tumejipanga vizuri kwa ajili ya msimu ujao na tunahitaji kuona kwamba matokeo ambayo tutapata yatakuwa ni mazuri kwetu.

"Kikubwa ni kuona kwamba tunamaliza msimu katika nafasi nzuri hatuhitaji kuona timu inakuwa kwenye presha ya kutaka kushuka daraja," amesema.

Msimu wa 2020/21 timu hiyo iliweza kucheza play off na timu ya Pamba FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza na iliweza kushinda jambo ambalo limeifanya iwe na uhakika wa kubaki ndani ya ligi msimu ujao.

Haikuwa kwenye mwendo mzuri kwa kile ambacho Juma Mgunda aliyekuwa Kocha Mkuu zama hizo kwa sasa ni Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi kwa kueleza kuwa waliwakosa nyota wao muhimu katika kikosi hicho ikiwa ni pamoja na Bakari Mwamnyeto ambaye aliibukia Yanga pamoja na Ibrahim Ame ambaye aliibukia Simba.

Usajili ambao wameufanya kwa sasa ni pamoja na ule wa Kocha Mkuu ambapo wanaye Melis Medo raia wa Marekani pia kipa ni yule Mussa Mbissa ambaye alikuwa ndani ya Mwadui FC.

Tayari imekwishacheza mchezo wa kirafiki na Simba SC kule Jijini Arusha na wakatoka suluhu ya bila kufungana 0-0.

Kwa misimu miwili ya hivi karibuni mwenendo wa Coastal Union sio wa kuridhisha na wadau wanaona alama hiyo haina kiashirio kizuri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live