Clatous Chama mchezaji ambaye ni mvivu, hakabi, anapoozesha timu na Kocha Robertinho anapaswa kumtupa benchi ameibuka tena kinara wiki hii baada ya kubeba bao bora pamoja na kuingia kikosi bora cha wiki huku sasa akipambania nafasi ya Mchezaji bora wa wiki kwenye Klabu Bingwa Afrika.
Ikumbukwe kuwa Mchezaji huyo mvivu na hafai kwenye soka la kisasa aliingia kikosi bora wiki mbili nyuma na alikuwa Mchezaji bora wa wiki pia, akitwaa na sasa itakuwa mara mbili mfululizo kwenye michuano hiyo.
Mchezaji huyo mvivu ana takwimu kali zaidi ligi ya ndani na sasa kimataifa, Watalaam wa mambo wanadai hiki anachokifanya kwenye hizi nafasi hakuna Mchezaji amewahi kufanya, ni namna nzuri sana ya Mchezaji anayepoozesha mpira kuonesha uwezo wake.
Neno moja kwa Mchezaji mvivu na asiyefaa kwenye soka la kisasa akiwa tu anatamba kwenye mechi dhidi ya Dar City na African Sports.
Mchezaji mvivu zaidi kwenye kikosi cha Simba ana mabao 15, kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika yupo kwenye orodha ya Wafungaji bora 10 wa muda wote barani Afrika kwenye michuano ya klabu bingwa.
Mvivu Clatous Chama ambaye hakabi anafungana mabao na nyota Yannick N’Jeng ambaye ni straika.
Kwenye orodha hiyo ya wafungaji 10 bora Afrika kuna Viungo washambuliaji wawili tu ambao ni Mohamed Aboutreika na Mvivu Clatous Chama.
Sisi ambao tunamkubali Kiungo huyu mvivu tunasema ni yeye tu na Mbwana Samatta ambao wamecheza Tanzania wapo kwenye orodha hiyo!
Tukisema ni Mchezaji bora wa muda wote kwanini hamtaki?