Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Clara kuweka heshima Saudia

Clara Luvanga Clara Luvanga.

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa kimataifa wa Tanzania kwa soka la wanawake, Clara Luvanga ana dakika 90 muhimu kesho katika pambano la dabi ya Ligi Kuu ya Wanawake ya Saudi Arabia wakati timu anayoichezea ya Al Nassr itakapoikabili Al Hilal, mchezo utakaoamua hatma ya ubingwa wa ligi hiyo kwa msimu huu.

Mechi hiyo itapigwa Uwanja wa Al Nassr, mjini Riyadh kuanzia Saa 2:00 usiku utazikutanisha timu hizo zinazochuana nafasi tatu za juu, chama la Clara likiongoza msimamo huku Al Hilal ikishika nafasi ya tatu.

Clara aliyetua kwenye timu hiyo msimu huu amekuwa na mchango mkubwa kwa timu hiyo inayoongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 28 kupitia michezo 10 ikishinda tisa na sare moja, huku wapinzani wao wakiwa nafasi ya tatu na pointi 16, huku Al Qadsiah ikiwa ya pili na pointi 17 ikicheza pia mechi 10 katika ligi hiyo yenye timu nane.

Ushindi wowote itakayopata A Nassr itaamanisha wanatetea tena taji kwa msimu wa pili mfululizo kwani itafikisha pointi 31 ambazo hazitaweza kufikiwa na timu yoyote kwani Al Qadsiah ikishinda mechi nne zilizosalia itafikisha pointi 29 tu, lakini kama itapoteza mbele ya Al Hilal itaichelewesha kusherehekea ubingwa hadi mechi zijazo.

Clara ndiye kinara wa mabao wa ligi hiyo akifunga 10 kati ya mabao 33 iliyfunga timu ya Al Nassr, akifuatiwa na Mtanzania mwenzake mwenzake, Enekia Lunyamila wa Eastern Flames akifunga sita katika mechi hizo 10 za ligi.

Akizungumza nasi kutokea Saudia, Clara alisema kutopoteza mchezo hata mmoja katika mechi 10 kunawapa mzuka wa kwenda kufanya vizuri mechi ya kesho ili kuchukua ubingwa.

"Kwa upande wangu naweza kusema nina jukumu kubwa kama straika kufunga, tunahitaji ushindi kwenye mchezo huo ili tutetee ubingwa kwa mara nyingine," amesema Clara nyota wa kimataifa wa Tanzania aliyewahi kuwika na Yanga Princess.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live