Straika wa zamani wa Yanga Princess, Clara Luvanga ambaye kwa sasa anakipiga Al Nassr ya Saudia ameanza vyema kwa kufunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Eastern Flames mechi ya Ligi Kuu wa Wanawake nchini Saudia.
Mechi hiyo iliwakutanisha ndugu wawili wa Tanzania Clara na Enekia Kasongo anayeitumikia Eastern Flames ya nchini humo.
Wote wawili jana ilikuwa kama vita kwani kila mmoja alipambana kuhakikisha anaipatia timu yake matokeo.
Ukiachana na hilo pia jana Clara alishinda tuzo ya WISAC Awards 2023 kwa wanawake wanaofanya vizuri katika mechi zilizofanyika Masaki jijini Dar es Salaam akiwashinda Fatuma Issa 'Fetty Densa' wa Simba Queens na Irene Kisisa wa Yanga Princess.