Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Clara Luvanga abeba tuzo Saudi Arabia

Clara Luvanga Goals Clara Luvanga

Sat, 30 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Mtanzania, Clara Luvanga kuchukua tuzo ya bao bora la mwezi Desemba nchini Saudia amewashukuru Watanzania kwa kumpa sapoti ya kumpigia kura.

Clara anachezea klabu ya Al Nassr inayoshiriki Ligi Kuu ya wanawake nchini humo alikuwa akiwania tuzo mbili ya mchezaji bora wa mwezi na bao bora alilofunga kwenye mechi dhidi ya Al Ittihad.

Akizungumza na Mwanaspoti kutoka Saudia, Clara alisema; "Nawashukuru sana Watanzania kwa mchango wao wa kunipigia kura najua haikuwa rahisi lakini walipambana hivyo nawaahidi sitawaangusha na nitaipeperusha vyema bendera ya nchi yangu," alisema staa huyo wa zamani wa Yanga Princess.

Tuzo hiyo alikuwa anachuana na wachezaji watatu na Clara aliwapiku wenzake kwa kupata asilimia 45.5, Veronica Perez (Al Qadisiah) akipata asilimia 12 na Ashleigh Plumptre wa Al Ittihad aliyepata kura za asilimia 42.5.

Kwenye tuzo ya mchezaji bora ilichukuliwa na Sarah Hamad wa Al Nassr aliyepata asilimia 58 akiwaacha Clara aliyepata kura 24.8 na Oriana Altuve aliyepata kura 17.2.

Mpaka sasa amecheza mechi saba za Ligi na kutupia mabao saba akitofautiana na Mtanzania mwenzake, Enekia Kasonga wa Eastern Flames aliyefunga mabao sita timu yake ikiwa ikishikilia nafasi ya pili kutoka mkiani mwa msimamo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live