Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Clara, Enekia wang'ara Ligi Kuu Saudia

Clara Luvanga Goals Clara, Enekia wang'ara Ligi Kuu Saudia

Tue, 26 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji wa timu ya taifa ya Wanawake ya Tanzania 'Twiga Stars', Clara Luvanga na Enekia Kasonga wameendelea kupeperusha vyema bendera nchi kwa kuongoza mbio za ufungaji bora kwenye Ligi Kuu Saudi Arabia msimu huu.

Luvanga na Enekia ambao wamejiunga na ligi hiyo msimu huu wote wapo kwenye mbio za ufungaji bora ambapo Luvanga anayeichezea Al Nassr inayoongoza kwenye msimamo wa ligi keshatupia mabao saba akiwa sawa na Oriana Altuve anayeichezea Al Shabab wakiwa kwenye nafasi ya kwanza.

Enekia anayeichezea Eastern Flames inayoshikilia nafasi ya pili kutoka mkiani akiwa na mabao sita sawa na washambuliaji wengine wanne.

Kwenye mabao hayo sita aliyofunga Enekia, matatu alifunga katika mchezo mmoja (hat-trick) dhidi ya Al Riyadh kwenye ushindi wa mabao 6-1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live