Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

City yafuata nyayo za Yanga mapema

Mby Cyt City yafuata nyayo za Yanga mapema

Fri, 2 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ili kuhakikisha Mbeya City inatambua na kuthamini mchango wa mashabiki wake, imeandaa mfumo wa kutoa kadi maalumu ikifuata ule unaotumiwa na Yanga, huku ikitangaza fursa kwa vijana 10 watakaoshindana kwenye ubunifu wa kutengeneza jezi za timu hiyo.

City yenye matawi 11 jijini Mbeya na mawili Dar es Salaam kwa sasa inapambana kuongeza idadi ya mashabiki baada ya mabadiliko ya uongozi yaliyofanyika hivi karibuni.

Mfumo wa kadi wa Yanga umeanza kujipatia umaarufu kutokana na mashabiki kuutumia kunufaika nao, ikiwamo katika huduma mbalimbali zikiwamo za kibeki.

Akizungumza leo Februari 1, Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Ally Nnunduma amesema katika kutambua mchango wa mashabiki wameamua kuandaa kadi ambazo zitakuwa zinamtambua kila mwanachama.

Pia amesema kutokana na kilio cha muda mrefu cha mashabiki na wadau wa soka jijini Mbeya kuhitaji Jezi, wametoa fursa kwa vijana 10 kuwasilisha ubunifu wa jezi ambapo mshindi ataondoka na zawadi.

"Hii timu siyo ya wanachama, bali ya mashabiki tumeamua kuwarudishia wao waamue nini tufanye kama uongozi, hatuoni sababu ya kupeleka tenda nje ya nchi ilhali wapo vijana wenye timu kuwaacha hivyo washiriki wote watapata zawadi ila kutakuwa na ile kubwa ya mshindi," amesema Nnunduma.

Amesema kadi hizo zinatarajiwa kuzinduliwa mwishoni mwa mwezi huu wa Februari ambapo kabla ya tukio hilo, uongozi utakutana na umoja wa matawi yote jijini Mbeya kusikiliza na kujadili mipango ya klabu.

Kwa upande wake, msemaji wa umoja wa mashabiki wa timu hiyo, Martine Geofrey amesema mashabiki wameamua kuendelea kuisapoti akieleza kuwa waliofikiria timu hiyo kutelekezwa na mashabiki hbaada ya kushuka daraja watasubiri sana.

Amesema kazi yao ni kushangilia na siyo kuzomea, na pia kuendelea kuipa nguvu timu hiyo nyakati zote na kwamba wana matarajio kufanya vizuri kwa City kwa mechi zilizobaki.

"Wengi waliamini tutaitelekeza timu baada ya kushuka daraja, lakini niwahakikishie tupo pamoja nyakati zote na kabla ya mechi ya Jumamosi dhidi ya Ken Gold tutakutana kikao cha pamoja kujadili mikakati ya mechi hiyo na nyingine zilizo mbele yetu," amesema Geofrey.

Chanzo: Mwanaspoti