Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

City yaamka, yainyoosha Pamba

Mbeya Ciyyy City yaamka, yainyoosha Pamba

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kucheza mechi tano mfululizo ushindi, hatimaye leo Mbeya City wameamka na kuichapa Pamba mabao 2-1 katika mchezo wa Championship.

Mechi hiyo ambayo ni ya raundi ya 10 kwa timu hizo, imepigwa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, ambapo licha ya pande zote kupambana kutafuta alama tatu, wenyeji waliweza kubaki na kicheko.

Pamba ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 14 kwa penalti kabla ya Eliud Ambokile kusaiwazishia City dakika ya 34 na kwenda mapumziko kwa nguvu sawa.

Kipindi cha pili City walionekana kurejea kwa kasi huku wakishangiliwa na mashabiki wao na dakika 79, Joseph Malaki aliweza kuiongezea bao la pili na kudumu hadi kumalizika kwa mechi hiyo.

Kabla ya mchezo huo, City ambayo ilishuka msimu uliopita ilikuwa na ukame wa ushindi kwani mara ya mwisho kupata pointi tatu ilikuwa Oktoba 1 ilipoilaza Ruvu Shooting bao 1-0 na sasa inafikisha pointi 14 na kupanda nafasi ya saba, huku 'TP Lindanda' wakibaki Top Four kwa alama 18.

Kocha msaidizi wa Pamba, Renatus Shija amesema baada ya kutangulia kupata bao, wachezaji walikosa umakini hadi kujikuta wakisawazishiwa na kufungwa la pili.

Amekubali wapinzani kuonesha ushindani akibainisha kwa sasa wanarudi Nyamagana jijini Mwanza kujipanga upya na mchezo ujao dhidi ya Ken Gold kuhakikisha wanashinda.

Chanzo: Mwanaspoti