Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chuku ajifunga mwaka Tabora United

Chuku Pict Chuku ajifunga mwaka Tabora United

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuikosoa Ligi Kuu kwa msimu mmoja na nusu, beki Salum Chuku amerejea baada ya kusaini mwaka mmoja kuitumikia Tabora United huku akiwa tayari kwa vita ya namba dhidi ya mastaa wa nje kwenye timu hiyo.

Chuku ambaye anacheza beki wa kushoto na winga, akitamba na Toto Africans, Mbeya Kwanza, Nkana Reds, KMC na Singida United, msimu uliomalizika alicheza First League akiwa nahodha wa Mwadui FC na kuipandisha Ligi ya Championship akifunga mabao mawili katika ushindi wa 5-2 dhidi ya Copco FC kwenye mchezo wa mtoano kuwania kupanda daraja.

Mbali na Chuku, tayari Tabora United ambayo imeweka kambi ya zaidi ya wiki tatu jijini Dar es Salaam inatajwa kumalizana na Makocha Wakenya, Francis Kamanzi na Yusuph Chippo imewasajili Haritier Makambo, Morice Chukwu, Yacouba Songne, Ally Makarani na Farhia Ondongo kuimarisha kikosi chao msimu ujao.

Chuku aliliambia Mwanaspoti kwa sasa yuko fiti asilimia 100 kushindana na kiu yake ni kucheza Ligi Kuu ndiyo maana akaachana na Mwadui na kwenda Tabora United na haogopi ushindani kwani anataka kuhakikisha anarejesha ubora wake na kuaminiwa na benchi la ufundi.

"Nimesaini Tabora mwaka mmoja nilikuwa na kiu ya kucheza Ligi Kuu na ndiyo daraja langu. Msimu uliopita nilicheza First League kwa sababu nilitoka kwenye majeraha na nilitaka kurejesha kiwango changu kwahiyo kwa sasa naona nimepona na kila kitu kiko sawa," alisema Chuku.

Alisema amerudi Ligi Kuu kufanya kazi na mashabiki wasiwe na wasiwasi kwani kazi atakayopiga wataiona, huku akitamba amejiandaa kufanya kazi na kutimiza majukumu yake kadri atakavyohitajika na benchi la ufundi na kuisaidia timu kufanya vizuri.

"Kwenye timu lazima kuwepo na ushindani mimi napenda changamoto nimejipanga kwa chochote kilicho mbele yangu kuhakikisha napata nafasi, nimekuja kufanya kazi watu wataiona kazi. Nimeshaungana na timu huku Dar es Salaam tuna wiki tatu tunafanya maandalizi yetu," alisema Chuku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live