Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Choppa ya Neymar yapigwa marufuku

Neymar Choppaaaaa Choppa ya Neymar yapigwa marufuku

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Supastaa Neymar ameshindwa kusafiri na helikopta yake yenye thamani ya Pauni 10 milioni baada ya kuzuiwa na mamlaka za anga Brazil. Kinachoelezwa, kibali kinachoruhusu chopa hiyo kufanya safari zake kimekwisha muda wake.

Na sasa, Neymar hataweza kutumia usafiri wake huo hadi hapo atakapopata kibali kingine na kwa kawaida kibali chenyewe hufika mwisho kila baada ya miaka mitatu. Helikopta hiyo imegharimu Pauni 10 milioni na ilinunuliwa na kampuni ya Neymar mwaka 2019. Supastaa huyo, huko nyuma alikuwa akimiliki helikopta nyingine mbili ikiwamo Cessna C yenye uwezo wa kubeba abiria 12.

Neymar anaripotiwa kuwa na pato kiasi cha Pauni 250 milioni na amekuwa akipatiwa zawadi ya vitu vya thamani kubwa huko Saudi Arabia baada ya kujiunga na klabu ya Al Hilal kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Sambamba na mkataba wa kulipwa Pauni 2.5 milioni kwa wili, Neymar amepewa pia magari manane ya kifahari ikiwamo Bentley Continental GP, Aston Martin DBX na Lamborghini Huracan. Amepewa pia nyumba na wafanyakazi watatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live