Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chivaviro aitosa Yanga, atua Kaizer Chiefs

Chivaviro Chivaviro aitosa Yanga, atua Kaizer Chiefs

Wed, 21 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dili la mshambuliaji Ranga Chivaviro kutua Yanga limeshatibuliwa baada ya klabu ya Kaizer Chiefs kumalizana naye juu kwa juu fasta.

Chivaviro alikuwa anawindwa vikali na klabu mbili za Tanzania, Azam na Yanga lakini mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Tanzania ndio waliokuwa wakiongoza mbio za kuwania saini yake.

Taarifa za uhakika ambazo Mwanaspoti imezipata kutoka klabu yake ya zamani ya Gallants iliyoshuka daraja ni kwamba tayari mshambuliaji huyo alishasaini mkataba wa awali wa miaka miwili na Chiefs.

Chivaviro alisaini dili hilo wiki mbili zilizopita ambapo sasa anasubiri hatua ya kuanza maisha mapya na klabu hiyo kongwe nchini Afrika Kusini.

"Alishasaini mkataba na Kaizer Chiefs nadhani bado hawajatangaza tu ila hataweza kuja tena Tanzania hilo nakuhakikishia," kilisema chanzo hicho cha ndani na kuongeza:

"Ni kweli Yanga walikuwa wanamtaka lakini naona ameshafanya maamuzi ya kubaki kucheza hapa Afrika Kusini wakati wowote watamtangaza."

Baada ya mshambuliaji huyo kutafutwa, alishindwa kukubali au kukataa akijibu kwa kifupi:"Kila kitu kinasimamiwa na meneja wangu nafikiri wakati ukifika mtajulishwa wapi nitakwenda," alisema Chivaviro.

Hatua ya Chiefs kuinasa saini hiyo ya Chivaviro itakuwa ni sawa na mshambuliaji huyo kumuwahi kocha Nasreddine Nabi ambaye naye yuko katika hatua za mwisho kutua klabu hiyo lakini ikionekana kuwa ni moja ya sababu ya kuzuia dili na Fiston Mayele kwenye timu hiyo.

Taarifa zinasema aliyekuwa kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi anatarajiwa kujiunga na timu hiyo mwanzoni mwa mwezi ujao, na inaelezwa kuwa amemtanguliza mshambuliaji huyo ambaye awali alitaka kumsajili Yanga kabla hajatangaza kuondoka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: