Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chirwa anukia Namungo

Chirwa Pic Data Obrey Chirwa (kushoto) akiwa katika majukumu yake uwanjani

Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Timu ya Namungo FC yenye Makao yake Rungwa Mkoani Lindi, haitaki utani msimu ujao kwani imeshaanza mazungumzo na wachezaji wazoefu wa ligi kuu Tanzania Bara ili kuwasajili lakini kubwa wakipambana kuipata saini ya Mshambuliaji wa zamani wa Azam na Yanga, Obrey Chirwa.

Chirwa kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na waajiri wake wa zamani Azam Fc na klabu hiyo kutokuwa na mpango wa kuongeza mkataba tena hivyo Namungo imeongeza kasi ya kutaka saini yake,wakiwa na Kumbukumbu nzuri ya kile alichokifanya katika misimu kadhaa nyuma.

Taarifa kutoka ndani ya Namungo zinasema viongozi wameweka mpango madhubuti katika kuhakikisha wananasa saini ya mshambuliaji huyo aliyemaliza Ligi Kuu Bara akiwa amefunga mabao matano msimu uliopita kwani wanaamini kuwa bado ana kiwango kizuri.

“Bado hatujamsajili ila tumeshaanza mazungumzo naye ili aweze kuwa mmoja ya wachezaji wetu msimu ujao, pia kuna wachezaji wengine ambao tumeshafanya nao mazungumzo na wengine tayari wameshasaini mikataba,” kilisema chanzo hicho.

Namungo ipo katika harakati za kutengeneza Kikosi chake kwa maandalizi ya Msimu ujao kwani msimu uliopita hawakufanya vizuri na kushindwa kupata nafasi ya kuliwakilisha taifa katika michuano ya Kimataifa.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz