Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chipukizi Msenegali asaka kiatu Afcon 2023

Lamine Camaraaaa Lamine Camara

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Bingwa mtetezi wa fainali ya Mataifa Afrika (Afcon 2023), Senegal imeanza vyema mashindano hayo baada ya kuichapa Gambia mabao 3-0 huku chipukizi wake Lamine Camara akifunga mabao mawili.

Lamine Camara (20) mchezaji bora chipukizi CAF 2023 ameibuka mchezaji bora wa mechi baada ya kufunga mabao mawili kwenye mechi hiyo huku bao la kwanza lifungwa na Pape Gueye.

Lamine alifanikisha Senegal kuchukua ubingwa wa Afcon chini ya miaka 20 na kuwa mchezaji bora wa mashindano hayo na ubingwa wa Chan 2022 na kuwa mchezaji bora wa mashindano.

Hadi sasa Lamine ndiye kinara wa mabao Afcon akiwa nayo mawili na mchezo unaofuta kwa Senegal ni dhdi ya Cameroon katika uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro nchini Ivory Coast Januari 19 mwaka huu.

Chanzo: Mwanaspoti