Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chippa United ya Afrika Kusini yatangaza kuishangilia Nigeria leo Afcon

Chippa United Ya Afrika Kusini Yatangaza Kuishangilia Nigeria Leo Afcon Chippa United ya Afrika Kusini yatangaza kuishangilia Nigeria leo Afcon

Wed, 7 Feb 2024 Chanzo: Mwananchi

Klabu ya Chippa United ya Afrika Kusini imewaacha mashabiki wa soka midomo wazi baada ya kutoa taarifa kuwa leo itakuwa inaishangilia Nigeria katika mchezo wa nusu fainali ya Afcon.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano na kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii ikisainiwa na Mwenyekiti wake, Siviwe Chippa Mpengesi, imeeleza sababu ya kufikia uamuzi huo ni kumpa sapoti golkipa wao, Stanley Nwabali anayechezea Nigeria.

Chippa United inashika nafasi ya 13 katika msimamo wa Ligi Kuu Afrika Kusini (PSL) ikiwa na pointi 18 baada ya kucheza mechi 16, ikishinda nne, kupoteza sita na kutoa sare sita.

Afrika Kusini itamenyama na Nigeria leo saa 2:00 usiku katika nusu fainali ya kwanza ya Mataifa ya Afrika (Afcon 2023).

Chanzo: Mwananchi