Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chipolopolo yaiwahi Lesotho Johannesburg

Image 304 960x640.png Chipolopolo yaiwahi Lesotho Johannesburg

Fri, 24 Mar 2023 Chanzo: Dar24

Saa chache baada ya kumaliza mchezo wa Mzunguko wa tatu wa Kundi H wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ dhidi ya Lesotho, kikosi cha Zambia ‘Chipolopolo’ kimefanya safari na kuwasili salama Afrika Kusini, tayari kwa mchezo wa Mzunguko wa nne wa kundi hilo.

Timu hizo zitarudiana tena Keshokutwa Jumapili (Machi 26) katika Uwanja wa Dobsonville mjini Johannesburg Afrika Kusini, huku Lesotho ikiwa mwenyeji wa mchezo huo.

Zambia imewasili Afrika Kusini ikishabihishwa na ushindi wa mabao 3-1 uliopatikana jana Alhamisi (Machi 23) katika Uwanja wa Levy Mwanawasa, mjini Ndola, huku mabao yakifungwa na Fashion Sakala, Lameck Banda aliyefunga mawili dakika ya 37, 53 na 57, huku Tshwarelo Bereng akiitanguliza Lesotho dakika 33.

Ushindi huo umeiweka kileleni Zambia kwa kufikisha alama 06, huku ikisubiri matokeo ya mchezo mwingine wa Kundi hilo kati ya Ivory Coast itakayokuwa mwenyeji wa Comoros katika Uwanja wa Bouaké, mjini Bouaké.

Ivory Coast ipo nafasi ya pili baada ya kucheza michezo miwili na kukusanya alama 04, huku Comoro ikiwa nafasi ya tatu kwa kufikisha alama 03 na Lesotho inaburuza mkia baada ya kujikusanyia alama 01.

Chanzo: Dar24