Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chilunda aing'arisha Azam FC Mapinduzi Cup

Azam Map Azam yashinda mchezo wake wa Kwanza Mapinduzi Cup

Wed, 5 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bao pekee la mshambuliaji Shaaban Iddi Chilunda limeipa mwanzo mzuri Azam FC katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Meli 4 City katika mchezo wa Kundi A usiku wa Jumanne Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Mechi iliyotangulia jioni, timu nyingine ya Bara, Namungo ilishinda pia 2-0 dhidi ya wenyeji wengine, Yosso Boys, Kundi A pia hapo hapo Uwanja wa Amaan.

Kiungo wa Azam FC, Frank Domayo ndie alieibuka nyota wa mchezo huo na kujinyakulia kitita cha Shilingi laki 500,000.

Mabao ya Namungo FC yamefungwa na Sixtus Sabilo dakika ya 53 na Relliant Lusajo dakika ya 90 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi sita kufuatia kuilaza Meli 4 City katika mchezo wa kwanza Jumapili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live