Beki wa kulia wa Azam FC, Nathaniel Chilambo amesema kwa sasa anapambana kuhakikisha anapewa muda mwingi wa kucheza katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo.
Hivi karibuni Uwanja wa Azam Comlex, Chamanzi alionekana mchezaji wa zamani wa Young Africans, Djuma Shaban akifanya mazoezi na kucheza mechi za kirafiki na timu hiyo na huenda akasajiliwa katika dirisha dogo.
Chilambo amesema anafahamu tetesi hizo na amejiandaa kufanya juhudi na kujituma zaidi ili kumuonyesha kocha anaitaka namba ya kikosi cha kwanza.
Amesema ushindani wa namba umemfanya apate dakika chache za kucheza mbele ya beki mwenzie, Lusa Mwaikenda ambaye ameonekana kufanya vizuri na kuiteka nafasi hiyo.
“Najua kinachoendelea lakini kwangu nafanya juhudi zangu na kujituma mazoezini na kwenye mechi ili nizidi kumuonesha mwalimu kuwa naitaka namba” amesema Chilambo.