Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chikwende aombewa muda zaidi kupiga kazi

Chikwende Pic Data Chikwende aombewa muda zaidi kupiga kazi

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KAIMU afisa mtendaji mkuu wa Mawanzi Market ya Morogoro, Mhibu Kanu ambaye pia kitaluma ni kocha na mchambuzi, ametazama  mshambuliaji wa Simba, Mzimbabwe Paferct Chikwende akagundua anahitaji muda zaidi ili kupata ujasiri wakuendana na kasi ya Ligi Kuu Bara.

Simba ilimsajili Chikwende akitokea klabu ya FC Platinum, baada ya kuonyesha kiwango cha juu kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika (Caf) baada ya kujiunga na Wekundu wa Msibazi, alicheza michuano ya Simba Super Cup na Kombe la Shirikisho Azam.

Kiwango alichokionyesha kwenye michezo hiyo, hakikuwashitua mashabiki wa Simba ambao walimtarajia angefanya maajabu kama yale aliyoyaonyesha wakati anacheza mechi za Caf.

Jambo ambalo Kanu amemkingia kifua na amemchambua Chikwende kupitia gazeti la Mwanaspoti Online leo Machi 24, 2021 kwamba anamuona  bado ni mchezaji mzuri ambaye ataisaidia Simba, isipokuwa anakosa kujiamini kutokana na ugeni wa timu.

"Mfano mzuri ni Rally Bwalya alisajiliwa akiwa kwenye kiwango cha juu zaidi, alipojiunga na Simba akawa kama ameshuka kiwango, badae amerejea kwenye makali yake na anategemewa kwenye kikosi hicho," amesema na amengeza kuwa;

"Chikwende akiyajua mazingira anayofanyia kazi na kuisoma ligi kuu ipoje, itamjenga na atakuwa mwiba zaidi kwa wapinzani wao, sidhani kama Simba ingemsajili kama angekuwa na kiwango kibovu," amesema.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz