Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chikwende, Lwanga kuonja balaa la Ligi Kuu

Chikwendeeee Data Chikwende, Lwanga kuonja balaa la Ligi Kuu

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Charles AbelMore by this AuthorBy Thobias SebastianMore by this Author Dar es Salaam. Nyota wapya waliosajiliwa na Simba, Perfect Chikwende na Taddeo Lwanga kwa mara ya kwanza wataonja ladha ya Ligi Kuu Tanzania Bara wakati timu hiyo itakapovaana na Dodoma Jiji FC katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, leo jioni.

Kusimama kwa Ligi Kuu Tanzania Bara ili kupisha maandalizi na ushiriki wa Taifa Stars kwenye mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Chan) kumesababisha nyota hao wachelewa kuichezea Simba kwenye ligi, lakini leo huenda wakaanza kuitumikia dhidi ya Dodoma Jiji.

Kiwango bora kilichoonyeshwa na wawili hao katika mashindano ya Simba Super Cup yaliyofanyika wiki iliyopita pamoja na kile cha Lwanga kwenye Kombe la Mapinduzi, kinatoa ishara kuwa nyota hao watakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kitakachoikabili Dodoma Jiji.

Kwanza ni kwa ajili ya kupunguza pengo la pointi baina yake na vinara wa Ligi, Yanga libakie pointi sita kwani kwa sasa Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 35, wakati Yanga wanaoongoza wana pointi 44.

Kwa vile Simba ina mechi tatu za viporo ili iwe sawa na Yanga kwa idadi ya michezo, ikiwa itapata ushindi leo na pia katika nyingine mbili dhidi ya Azam na Namungo FC, itafikisha jumla ya pointi 44 na kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi kwani itabebwa na utofauti wa mabao.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz