Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chico, Moloko Wamvurugia Nabi

CHIKO Moloko.png Chico, Moloko Wamvurugia Nabi

Sat, 19 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amesema kuwa kukosekana kwa wachezaji wake zaidi ya saba katika kikosi chake, kunamvurugia mipango ya ushindi kuelekea michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC).

Hiyo ni baada ya kuongezeka kwa majeruhi katika kikosi chake ambao ni Mkongomani, Jesus Moloko aliyeshindwa kumalizia mchezo wa FA dhidi ya Biashara United uliopigwa juzi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Yanga katika mchezo huo iliwakosa wachezaji saba, kati ya hao ni kutokana na majeraha ambao ni Yacouba Songne, Kibwana Shomari, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Chico Ushindi, Denis Nkane, Chrispin Ngushi na Dickson Job anayetumikia adhabu ya kufungiwa michezo mitatu.

Nabi alisema kuwa katika timu wanapokosekana wachezaji zaidi ya saba kunaharibu mipango ya kiufundi ya kocha katika kupata ushindi.

Nabi alisema kuwa kikosi chake kinakabiliwa na wachezaji wengi majeruhi, hadi unafikia wakati analazimika kuwatumia majeruhi kama ilivyokuwa kwa Moloko ambaye alimtumia akiwa ana majeraha katika mchezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live