Licha ya ubora mkubwa wanaouonyesha katika mechi zao, Chelsea wamelazimishwa sare ya 1-1 na Burnley katika mchezo wa Ligi ya England Uwanja wa Stamford Bridge Jijiji London.
Chelsea waliokuwa wanatafuta nafasi ya kushinda mechi ya tano mfululizo kwa mara ya kwanza chini ya Thomas Tuchel walionekana kama wanaelekea kuitengeneza rekodi hiyo japokuwa kwa muda, wakakaa kileleni kwa tofauti ya alama tano baada ya goli la Kai Havertz alilofunga dakika 12 kabla ya mapumziko. Matej Vydra aliisawazishia Burnley dakika ya 79.
Chelsea inafikisha pointi 26 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tatu zaidi ya Manchester City, wakati Burnley inafikisha pointi nane baada ya wote kucheza mechi 11.
Chelsea wamecheza huku wakiendelea kuwakosa washambuliaji wake Romelu Lukaku na Timo Werner.