Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea yatinga Robo Fainali Carabao

Kepa.jpeg Golikipa wa Chelsea, kipa Kepa Arrizabalaga aliokoa penati usiku wa jana

Wed, 27 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji Chelsea wamefanikiwa kutinga Robo Fainali ya Kombe la Ligi England, baada ya ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Southampton kufuatia sare ya 1-1 usiku wa Jumanne Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.

Kai Havertz alianza kuifungia Chelsea dakika ya 44, kabla ya Che Adams kuisawazishia Southampton dakika ya 47.

Katika mikwaju ya penalti, kipa Kepa Arrizabalaga aliokoa penalti ya Theo Walcott wakati Will Smallbone alipiga juu ya lango kuikosesha Southampton penalti mbili, wakati upande wa Chelsea Mason Mount pekee alikosa.

Waliofunga penalti za Chelsea ni Marcos Alonso, Callum Hudson-Odoi, Ben Chilwell na Reece James, wakati Adam Armstrong, Shane Long na Oriol Romeu ndio waliofunga za Southampton.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live