Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea yatakata San Siro, waichapa AC Milan bao 2

Auba Pierre.jpeg Mshambuliaji wa Chelsea Pierre-Emerick Aubameyang alipachika bao katika mchezo huo

Wed, 12 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chelsea imeibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya AC Milan katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya huku mlinzi wa zamani wa Chelsea Fikayo Tomori akionyeshwa kadi nyekundu ya mapema kabisa.

Tomori alimvuta jezi kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa England Mason Mount kabla ya refarii Daniel Siebert kuamua kuwa tuta na kadi nyekundu, tuta ambalo likafungwa na kiungo mkabaji wa Italia Jorginho kabla ya bao la Pierre-Emerick Aubameyang kufunga bao la pili kwenye mchezo huo

Ushindi wa Chelsea unaendeleza wigo wa ushindi kwa kocha mpya wa klabu hiyo Graham Potter sasa anafikisha mechi tano bila kupoteza.

Chelsea inaongoza kundi ikifuatiwa na RB Salzburg ambayo ilitoka sare ya bao moja kwa moja na Dinamo Zagreb

Chanzo: www.tanzaniaweb.live