Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea yashinda Villa Park

Jorginho Villa.jpeg Jorginho akishangilia goli alilofunga kwa mkwaju wa Penati

Mon, 27 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Chelsea imeonyesha kuimarika tena baada ya ushindi wa ugenini wa 3-1 dhidi ya wenyeji, Aston Villa katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Villa Park Jijini Birmingham.

Reece James alianza kujifunga dakika ya 28 kuipatia Aston Villa bao la kwanza, kabla ya Chelsea kuzinduka kwa mabao ya Jorginho , mawili na yote kwa penalti dakika ya 34 na 90 na ushei na mtokea benchi, Romelu Lukaku dakika ya 56.

Kwa ushindi huo, The Blues wanafikisha pointi 41 katika mchezo wa 19, ingawa wanabaki nafasi ya tatu, wakizidiwa tu wastani wa mabao na Liverpool ambao pia wana mechi moja mkononi.

Aston Villa ambayo ilicheza bila kocha wake, Steven Gerrard ambaye aliwekwa kando baada ya vipimo kuonyesha ameabukizwa virusi vya corona, inabaki na pointi zake 22 za mechi 18 katika nafasi ya 10.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live