Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea yaleta kipa mpya

Kiiiiii Chelsea yaleta kipa mpya

Thu, 1 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Chelsea imekamilisha usajili wa kipa Filip Jorgensen kwa ada ya Pauni 20.7 milioni akitokea Villarreal.

Kinda huyo wa Denmark amesaini mkataba wa miaka saba kwenye kikosi hicho cha The Blues na tayari ameshaanza mazoezi huko Atlanta.

Jorgensen alikuwa na msimu bora kwenye LaLiga baada ya kucheza mechi 36 akiwa na kikosi cha Villarreal. Katika mechi hizo, hakuruhusu bao kwenye mechi sita, huku akiokoa hatari 143 huku wastani wake wa kuokoa ukiwa chini ya asilimia 70.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 22 alijiunga na Villarreal miaka saba iliyopita akitokea kwenye akademia za GIF Nike na Malmo na kupita pia kwenye timu za Santa Catalina, Penya Arrabal na Mallorca. Baada ya kukamilisha uhamisho huo wa kutua Chelsea, Jorgensen alisema “ndoto zimekuwa kweli”, aliposema: “Huu uhamisho ni ndoto zilizotimia. Nimekoshwa na kitendo cha kusaini Chelsea, moja ya klabu kubwa duniani. Nasubiri kwa hamu kumfahamu kila mtu na kuanza kucheza na wachezaji wenzangu.”

Kipa huyo ni usajili wa sita kwa The Blues kwenye dirisha hili baada ya Marc Guiu, Caleb Wiley, Renato Veiga, Omari Kellyman na Kiernan Dewsbury-Hall. Miamba hiyo ya Stamford Bridge ilikuwa kwenye hatua za mwisho za kumfungulia mlango wa kutokea kiungo Conor Gallagher, anayeripotiwa kuwindwa na Atletico Madrid kwa dau lisilozidi Pauni 50 milioni.

Chanzo: Mwanaspoti