Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea yalazimishwa sare na Zenit, yamaliza nafasi ya Pili

Zenit Zenit walazimisha sare dhidi ya Chelsea

Thu, 9 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chelsea imeshindwa kumaliza kinara wa Kundi H baada ya kulazimishwa sare ya goli 3-3, mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Zenit St Petersburg mtanange uliopigwa Jumatano Disemba 8.

Chelsea ambayo wiki iliyopita walikutana kipigo cha goli 3-2 dhidi ya West Ham United walihitaji ushindi angalau kurudisha hali ya ushindi lakini haikuwa hivyo kwani timu zilienda mapumziko The Blues wakiwa nyuma kwa bao 2-1.

Magoli ya Chelsea kwenye mechi hiyo yamefungwa na Timo Werner aliyefunga bao mbili na mshambuliaji wa Ubeligiji Romelu Lukaku wote wakiwa wametokea kwenye janga la majeruhi.

Wakati mabao ya Zenit St Petersburg yamefungwa na Claudinho na Sardar Azmoun pamoja na lile bao la mtokea bechi Magomed Ozdoev.

Sare hiyo inaifanya Chelsea kumaliza nafasi ya pili nyuma ya vinara Juventus ambao wameshinda mechi ya mwisho dhidi ya Malmo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live