Southampton wamefanikiwa kuichapa Chelsea bao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu England mtanange uliopigwa Jumanne Agosti 30 dimba la St Mary’s ambapo watakatifu hao wakilazimika kutokea nyuma na kuibuka na ushindi muhimu.
Akiwa katika kikosi kipya, winga wa kimataifa wa England Raheem Sterling alikwamisha bao wavuni kunako dakika ya 23, goli ambalo limemfanya kuwa kinara kwenye upachikaji mabao klabuni hapo.
Lakini bao la Sterling lilifutwa na Romeo Lavia akimshinda ujanja mlinda mlango wa Chelsea na timu ya taifa ya Senegal Edouard Mendy kisha Adam Armstrong akamaliza mchezo kwa kufunga bao la ushindi kwa Southampton ambao mchezo uliopita alifungwa 1-0 na Manchester United.
Ushindi huo unaifanya kukwea mpaka nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu England ambapo wanafanana na Chelsea kukiwa na tofauti ya bao za kufunga na kufungwa.