Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea yajihakikishia kumnasa Kounde

Kounde Pic Data Jules Kounde

Thu, 21 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chelsea inaamini itanasa saini ya Jules Kounde, baada ya kuongeza ofa iliyofikai kitita cha Pauni 55 milioni, usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa ripoti Sevilla ipo tayari kupokea ofa hiyo, huku mazungumzo yakiendelea kufikia makubaliano.

Chelsea haikukata tamaa ya kupata saini ya Kounde, tangu mwaka jana ilipomfukuzia, lakini sasa beki huyo wa Kimataifa wa Ufaransa, anaelekea Stamford Bridge.

Wakati huohuo Kounde ameaga mashabiki wa Sevilla baada ya mazoezi ya mwisho, huku akiwa na matumaini ya dili lake kukamilika haraka iwezekanavyo.

Thomas Tuchel ameshaanza kuimarisha safu yake ya ulinzi kwa kumsajili Kalidou Koulibaly, akitokea Napoli kama mbadala wa Antonio Rudiger, aliyejiunga na Real Madrid.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live