Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea yaendeleza wimbi la ushindi, yaichapa Newcastle 3

E5863774 36DA 4530 896B 32A78DB296A8.jpeg Wachezaji wa Chelsea wakimpongeza Reece James

Sat, 30 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matajiri wa Jiji la London, timu ya Chelsea imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya England baada ya kuwachapa wenyeji, Newcastle United mabao 3-0 leo Uwanja wa St. James' Park .

Mabao ya Chelsea leo yamefungwa na beki wa kimataifa wa England, Reece James mawili dakika ya 65 na 77 na kiungo Mtaliano mzaliwa wa Brazil, Jorge Luiz Frello Filho ‘Jorginho’ dakika ya 81.

Kwa ushindi huo, The Blues inafikisha pointi 25 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi tatu zaidi ya Liverpool baada ya wote kucheza mechi 10, wakati Newcastle inabaki na pointi nne za mechi 10 pia katika nafasi ya 19.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live