Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea yaandamwa na majeruhi, watatu kuwakosa Watford

AZIP 696x498 Wachezaji wa chelsea wakabiliwa na majeruhi

Wed, 1 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel atafanya maamuzi dakika za mwisho kama Jorginho, Reece James na Timo Werner wanaweza kucheza dhidi ya Watford siku ya Jumatano The Blues wakiwa ugenini kwa mchezo wa Premier League.

Tuchel alisema wachezaji hao watatu walifanya mazoezi siku ya Jumanne na watakabiliana na vipimo kabla ya mechi hiyo itakayopigwa katika dimba la Vicarage Road.

Chelsea tayari ilikuwa na majeruhi watatu ambao ni Ben Chilwell, Mateo Kovacic na N’Golo Kante na kocha Tuchel amesema kikosi chake kitakuwa kikifuatilia kwa ukaribu kwa wiki zijazo.

“Itakuwa changamoto, lakini jambo zuri ni kwamba hapo awali ilikuwa na changamoto,” Tuchel alisema. “Hatubadilishi utaratibu wetu, tuna mawasiliano ya karibu na idara za matibabu na mazoezi ya mwili, na tunajaribu kutabiri mzigo na nani amezidiwa.

“Tutaangalia tunachohitaji katika michezo ijayo kuanzia hapo. Hatua kwa hatua. Ukiangalia mbele sana unaweza kuona wiki hizi zitakuwa ngumu, ndio maana tunaangazia undani, mchezo unaofuata na labda. michezo miwili iliyofuata.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live