Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea watinga Robo Fainali kibabe Ligi ya Mabingwa Ulaya

Chel X Dort.jpeg Chelsea watinga Robo Fainali kibabe Ligi ya Mabingwa Ulaya

Tue, 7 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vijana wa Graham Potter, klabu ya Chelsea wamefanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya baada ya kuitandika Klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani mabao 2-0 katika Uwanja wa Stamford Bridge.

Chelsea waliingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa bao 1-0 nchini Ujerumani katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza.

Huu ni ushindi wa tatu kwa Chelsea katika michezo 16 iliyopita , huku ukiwa ni ushindi wa pili mfululizo tangu walipofanya hivyo mwezo October.

Mabao yaliyoivusha Chelsea hatua ya Robo Fainali yamefungwa na Raheem Sterling alieweka mzani sawa na Kai Havertz aliepachika bao la 2.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live