Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea wapindua meza kibabe ugenini

Chelsea Vs Luton Chelsea wapindua meza kibabe ugenini

Sun, 8 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Chelsea imetoka nyuma na kuichapa Burnley FC mabao 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Jumamaosi Uwanja wa Turf Moor mjini Burnley.

Mshambuliaji Mfaransa, Wilson Odobert alianza kuifungia Burnley dakika ya 15, lakini beki Mbelgiji Ameen akajifunga dakika ya 42 kuisawazishia Chelsea, kabla ya C. Palmer kufunga la pili kwa penalti ya 50, Raheem Sterling la tatu dakika ya 65 na Nicolas Jackson la nne dakika ya 74.

Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi 11 na kusogea nafasi ya 10, wakati Burnley inabaki na pointi zake nne nafasi ya 18 baada ya wote kucheza mechi nane.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live